The House of Favourite Newspapers

Modric Ataka Kumaliza Soka Lake Madrid

0

KIUNGO wa Real Madrid, Luka Modric, ameendelea kusema anataka kuona anamalizia kipindi chake cha kucheza kwenye kikosi hicho akiwa amebakiwa na miezi nane katika mkataba wake na timu hiyo Hata hivyo, bado kiungo huyo amekuwa akitajwa kuwa anaweza kujiunga na Tottenham Hotspur mwishoni mwa msimu huu.

 

Mshindi huyo wa Ballon d’Or 2018, inaelezwa kuwa, bado ana muda wa kucheza zaidi kwa msimu mmoja kabla hajatundika daruga ambapo hivi sasa ana miaka 35. “Bado najisikia vizuri sana, suala la michezo ambayo sijacheza nafikiri haya ni maamuzi ya kocha na
siyo mimi, kama ikitokea natakiwa kucheza nitaitumikia timu yangu kwa moyo wote.

 

Naona miguu yangu bado inaniruhusu kucheza sana, lakini ngoja tuone nini kitatokea. “Nimekuwa nikisema mara nyingi na narudia
kusema kuwa ninataka kuona namalizi akipindi changu cha soka hapa,” alisema

 

Leave A Reply