The House of Favourite Newspapers

Mojabet Yadhamini fainali za Bongo Star Search (BSS)

KAMPUNI ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha kupitia mmoja ya michezo yake ya Boompesa leo imetangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search (BSS) ambazo zinatarajiwa kufanyika Disemba 22 mwaka huu.

 

kizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza kudhamini Bongo Star Search msimu wa 9, Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya Mojabet Diana Chacha alisema kuwa wameona ni muhimu kushirikiana na Bongo Star Search ili kuendelea kuimbua vipaji vipya vya muziki hapa nchini na pia kufanya vijana zaidi waweze kujiajiri kupitia muziki.

 

Sisi lengo ni kuwafanya Watanzania wengi waweze kujiajiri kupitia zawadi za fedha taslimu ambazo huwa tunawapa washindi wetu. Kwa maana hiyo tumeona ni muhimu kutanua wingu wetu na kuelekeza kwenye muziki kwani huko pia kuna vipaji vyingi lakini kutokana na kutopata nafasi ya kuonekana, tunaamini kuwa ushirikiano wetu na BSS utaweza kutanua wingu na kufikia Watanzania wengi na hasa kupitia vijana kupitia Boompesa, alisema Chacha.

 

Chacha aliongeza kuwa Boompesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea.

 

Mojabet ni kampuni ya michezo ya Bahati na sibu na Boompesa ni mmoja ya michezo yetu. Mojabet kupitia Boompesa ni wadhamini wakuu katika Bss season 9 na  nusu fainali na fainali Boompesa imeandaa zawadi nono na sio kwa washiriki wa bss tu bali hata kwa wachezaji wa mchezo huo kwa kupitia code ya Bss. kwani kuna TZS 50 milioni imeandaliwa kwa wachezaji hivyo ni fursa kwa kila mtu kucheza zaidi ili kujiongezea nafasi yake ya kushinda.

 

Kwa upande wake, Mratibu na Jaji Mkuu wa Bongo Star Search Rita Paulsen alisema kuwa fainali za mwaka huu zitakuwa tofauti na za miaka iliyopita kwani mshindi, mbali na kujipatia fedha taslimu lakini pia ataweza kupata ajira kutoka kwa kampuni ya Mojabet.

 

Rita alisema kuwa Mojabet kupitia Boompesa wamefanya fainali za mwaka huu ziwe za kipekee, na  akiongeza kuwa mshindi wa BSS msimu wa tisa atapata fedha taslimu milioni tano, vile vile atakuwa Balozi wa Boompesa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo atakuwa analipwa shilingi milioni mbili kwa mwezi.

 

Tumeingia mkataba wa mwaka na kampuni kubwa ya muziki ambayo itakuwa ikizalisha na kusambaza kazi za mshindi wa mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

Lengo ni kuhakikisha mshindi wetu anakuwa ni staa kweli, alisema Rita huku akitoa shukrani kwa kampuni ya Mojabet kupitia Boompesa kuweza kudhamini mashindano ya mwaka huu ambayo yamekuwa tofauti na ya miaka ya nyuma.

Vile Vile, aliongeza kuwa wakati wa kilele cha fainali hizo kutachezeshwa mchezo wa Boompesa ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini.

 

 

Comments are closed.