The House of Favourite Newspapers

Msaga Sumu Nina Mke, Acheni Shobo!

Selemani Jabir ‘Msaga Sumu’.

NGULI wa Muziki wa Singeli, Selemani Jabir ‘Msaga Sumu’, amewakata ngebe wanawake ambao wamekuwa wakimshobokea wakati yeye ana mke na watoto wawili.

 

Akizungumza na Full Shangwe, Msaga Sumu anayebamba na Ngoma ya Mwanaume Mashine alisema kuwa hana mpango na wanawake wanaomshobokea na haitakuja kutokea kwani ana ndoa yake anayoipenda.

 

“Imekuwa kero sasa, ninachoweza kuwaambia ni kwamba wanawake waache kunishobokea, Kwanza watambue kuwa ninaipenda familia yangu na kwa sasa ninatimiza miaka nane ya ndoa yangu, na nina watoto wawili, inshallah Mungu kanijalia,”alisema Msaga Sumu na kuongeza;

 

“Kwa sasa najipanga kuzindua rasmi Mwanaume Mashine ndani ya Dar Live hivyo soon nitatangaza.

Stori: Jacqline Oisso

Comments are closed.