Msanii Shilole Alipuka Gharama ya Mwili Wake, Atoa Elimu Kwa Mastaa

MWIGIZAJI na msanii mkali anapokuwa mbele ya kamera, Zuwena Mohammed ‘Shilole ‘ ameamua kuwahamasisha mastaa na watu mbalimbali kuepuka gharama ya kujitengeneza badala yake wanaweza kubaki na uhasili wao na wakapendeza.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Shilole alisema, amejitathmini na kugundua kuwa hatumii gharama kubwa kununua nywele za bei mbaya au kutumia madawa ya usoni, lakini bado anaonekana mrembo.
“Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu,” alisema Shilole
Stori; Khadija Bakari, Dar
 
			
