The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Kwanza Spoti Xtra Akabidhiwa Beats by Dre Orijino – Video

Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Michael Mombuli (kulia) akimkabidhi mshindi wa Headphones za Beats by Dre, Yohana Malilika.

 

TIMU ya Simba imefanikiwa kuwa ya kwanza kutoa mshindi wa Headphones za kijanja za Beats by Dre katika shindano linaloendeshwa na gazeti bora kabisa la michezo hapa nchinila Spoti Xtra ambalo uwa mtaani kila siku ya Jumapili.

 

Yohana Malilika ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya Simba na anayevutiwa zaidi na uchezaji wa Shiza Kichuya ndiye amekuwa mtu wa kwanza kujishindia Headphones za Beats by Dre baada ya kuibuka mshindi katika droo ya shindano lililofanyika Alhamisi hii kwenye kipindi cha michezo cha Spoti Hausi kinachorushwa kupitia Global TV Online kila Alhamisi saa 10:00 jioni.

 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Headphones hizo na Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Michael Mombuli katika ofisi za Gazeti hilo zilizopo Sinza Mori, Dar, Malilika ambaye ni mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam na anayejishughulisha na kazi ya kutengeza garden alisema kuwa, katika maisha yake hakuwa na matarajio ya siku kumiliki headphones za kijanja kama hizo ambazo ni orijino kutoka nchini Marekani.

 

“Hakika nashukuru sana Mungu  kwani sikuwa na matarajio ya siku moja kumiliki kitu kama hiki ambacho ni Orijino, niwaombe tu Watanzania wote kushiriki bahati nasibu hii kwani hakuna upendeleo wowote, zile habari za kusema kuwa wanapeana wenyewe hazina ukweli wowote.

“Binafsi sikuwa na mtu yoyote ambaye ananijua Spoti Xtra lakini nimeibuka mshindi wa headphones za kijanja kabisa,” alisema Malilika ambaye pia shabiki mkubwa wa Manchester United ya nchini Uingereza.

 

Shindano bado linaendelea, nunua #SpotiXtra kila Jumapili ushinde. Kadri unavyoshiriki zaidi ndiyo unapata nafasi kubwa ya kuibuka mshindi.
Nunua #SpotiXtra Jumapili hii na kila Jumapili.

Mwandishi wetu.

 

SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.