The House of Favourite Newspapers

MSIGWA: Tunapiga Makofi, Hakuna Pesa Tusidanganyane Hapa! – Video

MBUNGE wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, akichangia hoja katika mjadala wa  Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 amesema hakuna haja ya kuipongeza Serikali kwa mambo inayofanya kwani imesababisha uchumi umeporomoka na hakuna pesa mikononi mwa wananchi.

 

Msigwa amemvaa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, akimtaka aeleze ni uchumi wa aina gani anaoumini huku akidai kwamba baadhi ya mambo anayoyatekeleza kwa sasa ni tofauti na alivyokuwa akifanya enzi za uongozi wa Rais Kikwete. 

 

“Siwezi kuipongeza Serikali kwa sababu imeporomosha uchumi, hakuna pesa kwenye mifuko ya wananchi, enzi za Mkapa na Kikwete uchumi ulikuwa unavutia wawekezaji, lakini uchumi huu wawekezaji wanaonekana ni wezi, wakwepa kodi.

 

“Tunaua Serikali za Mitaa, makusanyo yote yanaenda Serikali Kuu, huku chini kunabaki maumivu tu, tunakopa pesa nyingi, uchumi unakwenda kuzama, tunapongezanapongezana tu. Huu ndiyo wakati ambao ilitakiwa Bunge lionyeshe nguvu yake kwa Serikali. Kwa nini Serikali hii inaanzisha miradi bila kupitishwa na Bunge?” alisema Msigwa.

VIDEO: MSIKIE MSIGWA AKIFUNGUKA

Comments are closed.