The House of Favourite Newspapers

MSIMU MPYA WA KILI MARATHON WAZINDULIWA

Mkurugenzi wa Executive Solution, Aggrey  Marealle,  akiwakaribisha wageni rasmi katika uzinduzi wa Kili Marathon.

WADHAMINI wakuu wa mbio ndefu, Kampuni ya bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro, leo wamezindua msimu mpya wa mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Moshi mkoani Kiliamanjaro na kufikia kilele Machi 3 mwakani.

Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Bia ya Kilianjaro. Pamela Kikuli. ambaye bia yake imedhamini mashindano hayo akiongea na wageni waalikwa.

Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, ambaye aliwataka Watanzania kujiandaa na kushiriki vyema mashindano hayo ili kufuta aibu ya wageni kuzoa tuzo mbalimbali za mashindano hayo na wao kubaki wasindikizaji kila mwaka.

Matukio katika Picha:

Katibu wa Chama cha Riadha  Tanzania, Filbert Bayi, akiongea kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini, Anthony Mtaka, akiongea machache kabla ya kumpisha mgeni rasmi.
Mwakyembe akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo ambayo alisema yana umuhimu mkubwa kwa kuimarisha afya na kujenga mahusiano na washiriki wa nchi mbalimbali.
…Akimpa Pamela zawadi ya picha inayoashiria utalii kutokana na bia yake kudhamini mashindano hayo kwa miaka 17 mfululizo sasa.
Mkuu wa Masoko wa Tigo, William Mpinga, alikabidhiwa zawadi hiyo kwa kuwa mdhamini mwenza kwenye msimu huu na misimu kadhaa iliyopita.
Mwakyembe akikata keki baada ya uzinduzi huo.

Wanahabari wakiwa kazini katika uzinduzi huo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

 

Comments are closed.