The House of Favourite Newspapers

Msudani wa Simba ampagawisha kocha Mwarabu

KOCHA wa viungo wa klabu ya Simba, Adel Zrane amefurahishwa na uwezo mkubwa alionao beki mpya wa Simba raia wa Sudan Shiboub Sharaf Eldin aliyetua Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Al-Hilal ya Sudan.

 

Zrane amesema anafurahishwa na uwezo wa kukaba na kucheza kwa nidhamu alionao Eldin na kukiri kuwa endapo atadumu kweye kiwango hicho kwa msimu mzima basi atakuwa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi ya simba.

 

“Nimemuangalia Eldin kwa muda huu mchache tuliokaa huku Afrika Kusini nimegundua ana uwezo mkubwa sana wa kukaba na kutumia nidhamu ya hali ya juu katika kila tukio, kiukweli nimefurahishwa sana na uwezo wake, endapo atakuwa fiti kwa msimu mzima basi atakuwa msaada mkubwa kwetu,” alisema Zrane.

Comments are closed.