MTANGAZAJI AFICHUA SIRI KUALIKWA NDOA YA AY

Shaffie Weru.

ZIKIWA zimepita siku tatu tangu mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu aitwaye Remmy mwenye asili ya Rwanda, mtangazaji maarufu wa redio nchini Kenya, Shaffie Weru amefichua siri ya kualikwa katika ndoa hiyo.

 

Katika mahojiano ya Shaffie na mtandao wa Global Publishers kabla ya kuhudhuria ndoa hiyo, Shaffie alisema AY alizingatia ndoa yake kuwa ya siri na kuamua kuwaalika watu wake wa karibu pamoja na familia yake.

 

AY na mkewe.

 

“Nilimfahamu AY kwenye kazi zangu za utangazaji, ni zaidi ya miaka 10 sasa. Tumesafiri pamoja kwa muda mrefu, tumefanya biashara wote na vingine vingi. AY amenisaidia sana kujulikana nchini mwao (Tanzania) na mimi kumtam­bulisha zaidi Kenya na ndiyo sababu ya kualikwa kwangu kwenye ndoa yake,” alisema Shaffie.

 

AY alifunga ndoa Jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Golden Tulip, Rwanda na kuhudhuriwa na mastaa wachache akiwemo meneja wa Diamond, Sallam, MwanaFA pamoja na mtangazaji B12.

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment