The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA GODZILLA AWATOA WATU MACHOZI

 

INAUMA sana! Mbali na waombolezaji kuguswa na kifo cha Rapa Golden Mbunda ‘Godzilla’, mtoto pekee wa marehemu ait­waye Shawn amewaliza wengi wakati wa mazishi ya msanii huyo.

Tukio hilo lililogusa hisia za wengi lilitokea Jumamosi iliyo­pita nyumbani kwa marehemu, Salasala-Mbezi jijini Dar.

Mamia ya waombole­zaji waliofika kwa ajili ya kum­sindikiza marehemu Godzilla katika makao yake ya milele, walionekana kulizwa zaidi na mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3.

“Kwa kweli mtoto huyu anawaliza wengi, anaonekana anaelewa kila kitu kinachoende­lea licha ya kuwa umri wake ni mdogo, anahuzunisha,” alisikika mmoja wa waombolezaji.

 

Waombolezaji wengi waliofi­ka msibani hapo, walionekana kuguswa zaidi na mtoto huyo hususan pale alipokuwa akiaga jeneza la baba yake katika Uwanja wa Salasala.

Akizungumza msibani hapo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema marehemu Godzilla wakati wa uhai wake, alimpa mama yake mzazi shilingi milioni nne, na kuahidi kumuongeza shilingi milioni moja kama mtaji ili afun­gue duka la madawa.

“Hata hivyo, pesa hizo mama mtu alilazimika kuzitumia kumtibia marehemu Godzilla alipokuwa anaumwa hivyo na mimi nimeguswa na hili, nitamrejeshea shilingi milioni tano, Fid Q utaniona ili uweze kumkabidhi mama,” alisema Makonda.

Mwili wa Godzilla ulizikwa Ju­mamosi iliyopita katika Maka­buri ya Kinondoni jijini Dar.

Mbali na Makonda na wasanii mbalimbali kujitokeza katika mazishi hayo, viongozi wen­gine waliokuwepo ni pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof Jay’.

Comments are closed.