The House of Favourite Newspapers

Kilichojiri Mahakamani… Mume Anayedaiwa Kumuua Naomi

UPANDE wa Jamhuri leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umesema upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe, Naomi Marijani, upo katika hatua za mwisho kukamilika.

 

Akiiambia mahakam hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amemweleza Hakimu Mkazi, Salum Ally, kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua nzuri na za mwisho kukamilika. Wankyo ameomba shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande. Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo anadaiwa alilitenda Mei 15, 2019, katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam alipomuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.

 

Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa kisha kuyafukia shambani majivu ya mwili wa marehemu.

Imeandikwa na Denis Mtima | @globalpublishers.

Comments are closed.