Muuaji Nchini Marekani Auawa Licha ya Ombi Kutoka kwa Muathiriwa Kutaka Kumuokoa

MFUNGWA Nchini Marekani aliyejulikana kwa majina Joe Nathan James, ambaye alimuua mpenzi wake wa zamani Miongo kadhaa iliyopita amenyongwa.
Mfungwa huyo amechomwa Sindano ya sumu kwenye Jela ya Kusini mwa Alabama baada ya Mahakama kukataa ombi hilo la kuzuiliwa kunyongwa kwa mfungwa huyo.
James alipatikana na hatia ya mauaji ya kumuua Faith Hall (26) aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1994, katika jiji la Birmingham.

Mabinti wawili wa Faith Hall, walitakaa mzee huyo wa miaka 50 atumikie kifungo cha maisha Jela badala ya kunyongwa.
Waendesha Mashtaka walisema kuwa James alichumbiana na Faith Hall kwa muda mfupi na kumshawishi kwa miezi kadhaa kabla ya kumuua.
Agosti 15, 1994 Faith Hall alikuwa kwa rafiki yake ambapo James aliingia ndani akachomoa Bunduki kutoka kiunoni mwake na kumpiga Faith Hall risasi mara tatu ambapo ilisababisha kifo cha mwanamke huyo kulingana na hati za Mahakama zinavyodai.

