The House of Favourite Newspapers

Mwana, Niva Bifu Zito

Mwanaheri Ahmed ‘Mwana

WAIGIZAJI wa Bongo Movies, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ na Zuber Mohamed ‘Niva’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito, kisa kikitajwa kuwa ni msanii mwenzao, Riyama Ally.

Uchunguzi wa Za Motomoto News ulibaini kwamba, wawili hao wako kwenye bifu kwa zaidi ya miaka miwili sasa baada ya Niva kumkanya Mwana kuhusu suala la kumtukana na kumsema vibaya msanii mwenzake, Riyama ambaye ndiye aliyemtambulisha kwenye sanaa.

Zuber Mohamed ‘Niva’

Alipotafutwa Niva kuhusu ishu hiyo alisema kuwa, ni kweli hayupo vizuri na Mwana kutokana na kumrekebisha kwamba aache tabia ya kumsema vibaya na kumtukana Riyama ambaye ndiye alimtambulisha kwenye sanaa ya filamu na mpaka leo hawako vizuri.

Kwa upande wake Mwana alisema: “Sijawahi kumtukana Riyama na huyo Niva hajawahi kunirekebisha chochote ila siko naye karibu kwa sababu siyo rafiki yangu.”

Comments are closed.