The House of Favourite Newspapers

Mwana Ukome Kinawaka Kinesi

0

PAMBANO la Dar Boxing Derby linatarajia  kupigwa Oktoba 30 mwaka huu kwa mabondia Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ dhidi ya Adam Kipenga na kupigwa kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar ambalo itakwenda kwa jina la Mwana Ukome baada ya kuzinduliwa leo Ijumaa kwenye  Uwanja wa  Las Vegas uliopo Mabibo, Dar.

 

Huu ni msimu wa pili kufanyika kwa pambano la Dar Boxing Derby ambapo pia Idd Pialali atapanda ulingoni dhidi ya Ramadhan Shauri wakati Seleman Kidunda akipanda ulingoni kuzichapa na Jacob Maganga wa Tanga huku Ismail Galiatano akitarajia kumaliza utata na Allan Kamote na Haji Juma akimaliza na George Bonabucha.

 

Wengine ni Hassan Ndonga dhidi ya James Kibazange, Grace Mwakamele na Happy Daud Halima Vunjabei mpinzani wake anatarajia kuwekwa wazi wakiwemo mabondia wengine watakaopanda ulingoni.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, promota wa pambano hilo, Kapteni Seleman Semunyu alisema kuwa awali pambano hilo lilipangwa kufanyika kwenye Ufukwe wa Kidimbwi lakini kutokana na maombi ya mashabiki wengi sasa litapigwa kwenye Uwanja wa Kinesi Dar.

“Dar Boxing Derby ambayo itaenda kwa jina la. Mwana Ukome litapigwa hapa Kinesi badala ya Kidimbwi kutokana na maombi ya wadau wengi  ambao wakati wote wamekuwa wakitupa sapoti kubwa katika mapambano yetu.

 

“Niwaambia tu kwamba Chichi Mawe na Kipenga, Ramadhan Shauri na Idd Pialali, Bonny Sela na Sadick Momba lakini Seleman Kidunda na Jacob Mangaga, Allan Kamote na Ismail Galiatano, George Bonabucha akitarajia kucheza na Haji Juma hii ni kwa ajili ya wadau wangu ambao wamekuwa sapoti kubwa kwetu Peak Time Media katika kazi zetu,” alisema Kepteni Semunyu.

Stori: Ibrahim Mussa

Leave A Reply