The House of Favourite Newspapers

MWANA: USTAA MWISHO GETINI

Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ ameibuka na kueleza kwamba ustaa wake unaishia getini na hauingii kwenye ndoa yake ili usije kuivunja kama ilivyozoeleka kutokea kwa mastaa wenzake.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Mwana alisema ndoa nyingi za mastaa hazidumu kwa sababu wanaupeleka ustaa huo mpaka ndani, jambo ambalo kwake halipo kwani amejiwekea kuwa akishafika kwenye geti la nyumbani kwake anauacha hapo, akiingia ndani anaingia kama mke wa mtu.

“Kikubwa ninamuomba Mungu kwa ajili ya ndoa yangu pia vingine ninavyovifanya ni kumuheshimu mume wangu, kumpenda, kumthamini na kumjali hivyo maisha yangu nikiwa nje ya nyumbani ni tofauti na ya ndani,”

Stori:Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.