The House of Favourite Newspapers

Mwanachuo Amuuwa Mpenzi wake kwa Kisu Kisa Wivu wa Mpenzi Dodoma

0
Kamanda wa Polisi Dodoma

MWANAFUNZI wa Chuo cha St John, Winfrida Michael (24) amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julius Gervas (26) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 7,2022 baada ya Julius kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma.

Ofisa muuguzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ester Ngoloki amesema walimpokea Julius akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply