The House of Favourite Newspapers

MwanaFA ndo’ Kishazima Bifu na AY

0

MWANA-FA-12Muziki wa Hip Hop Bongo, Khamis Mwijuma ‘Mwana FA’.

Boniphace Ngumije
SAMBAZA NA HII SASA! Baada ya ubuyu mzito kusambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa maswahiba wanaofanya Muziki wa Hip Hop Bongo, Khamis Mwijuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yessaya wako katika bifu zito baada ya FA kutoa ngoma ya Asanteni Kwa Kuja inayosemekana ina vijembe kwa AY, hatimaye FA ameibuka na kuuzima ubuyu wa bifu hilo.

11665642_10155977768540413_4151347418411606052_nAmbweye Yesaya ‘AY’

Baada ya kupenyezewa kishkaji ubuyu huo, Ubuyu wa Town ilimsaka FA ambaye baada ya kusomewa mashtaka yake akadai kwamba hakuna bifu lolote lile na hata hiyo ngoma aliyoiachia haikuwa na mistari yenye kuudhi kwa AY, ila kwa wasikilizaji sasa, ndiyo imepokelewa kivingine.

“Mimi na AY ni washkaji, hatuwezi kutofautiana na kupigana vijembe, tupo pamoja tukila gudi taimu nawashangaa wanaovumisha kwamba tuna bifu,” alisema FA na kupiga full stop.

Leave A Reply