The House of Favourite Newspapers

Mwanahawa Ally, Sabaha, Wasepa Na Kijiji Usiku Wa Marashi

Muim wa Taarabu, Sabaha Salum Muchachu, akiburudisha kwenye usiku huo wa Marashi.

 

USIKU wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa King Solomon, jijini Dar kulikuwa na shoo ya Usiku wa Marashi na Kudamshi, ambayo iliwakutanisha nguli na Muziki wa Taarabu Bongo na mashabiki wa muziki huo ambao waliburudika na miondoko ya Pwani, vyakula na marashi yaliyotawala ukumbini hapo.

Mashabiki waliofurika kwenye shoo hiyo

Kwenye shoo hiyo, walioangusha burudani ya nguvu na kusepa na kijiji walikuwa Nassor Cholo, Sabaha Salum Muchachu, Mwanahawa Ally, Rukaiya na wengine wengi.

Mwanahawa Ally akikinukisha kwenye shoo hiyo.

 

Shoo hiyo iliandaliwa na mwanadada mjasiriamali Tahya Salum ‘Shantee’ ambaye alisema madhumuni ya kuandaa shoo hiyo ni kurudisha Muziki wa Taarab asilia juu kama ilivyokuwa zamani.

Nassor Cholo naye hakuwa nyuma kuwaburudisha mashabiki wa Taarabu

“Unajua kwa sasa Muziki wa Taarab ya kisasa ndio unapewa nafasi sana, lakini Taarab ile asilia haina nafasi, mimi nimeamua kuurudisha kwa mashabiki na matamasha haya yatakuwa endelevu kwani baada ya hapa tutakwenda Tanga, Zanzibar na mikoani,” alisema Tahya.

Mashabiki wa Taarabu wakizidi kufurahia shoo hiyo ya Usiku wa Marashi na Kudamshi.

 

Stori: Boniphace Ngumije | GPL

 

Comments are closed.