The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Amuua Mumewe, Amzika Kimyakimya!

MWANAMKE mmoja nchini Uganda, Dina Ainomugisha (45) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mume wake, Gordon Ahimbisibwe na kumzika kwa siri huku akishirikiana na ndugu zake kwa kinachodaiwa ni ugomvi wa mali za familia.

 

Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ibanda, Rogers Chebene amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa ambaye alishiriki katika zoezi hilo aliamua kutoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji baada ya kukosa mgao wake wa fedha kama walivyokubaliana awali.

 

Baada ya kumuua, watuhumiwa wote wakishirikiana, walichimba shimo na kuuzika mwili wa marehemu usiku wa manane.

 

Watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo wametajwa kuwa ni Keresensio Mwesigye ‘Kamwesi’, Experito Kacunguza, Stephen Mukama na Medrine Kabasiita ambao wote wameshakamatwa na jeshi la Polisi.

 

Taarifa zimeeleza kwamba, mwili wa Marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Ruhoko kwa uchunguzi zaidi.

 

“DIAMOND ni Freemason, Siwezi Kwenda WASAFI” – G BWAY

Comments are closed.