The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Aweka Rekodi Kuendesha Ndege ya Kivita

AVANI Chaturvedi (24), ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuendesha ndege ya kivita akiwa peke yake nchini India baada ya kuendesha ndege aina ya Mig-21 Bison kwa dakika 30 wiki iliyopita.

 

Chaturvedi alikuwa miongoni mwa wanawake watatu wa kwanza marubani wa ndege za kivita kujumuishwa katika jeshi la wanaanga nchini India ambapo jeshi hilo lilichapisha picha yake akiwa amesimama karibu ndege ya hiyo.

Mwanamke huyo alifuzu mafunzo ya kurusha ndege hizo Juni, 2016  na wanawake wengine wawili, Bhawana Kanth na Mohana Singh, ambao wataendesha ndege kama hiyo hivi karibuni kama sehemu ya mafuzo.

 

Kabla ya mwaka 2016, wanawake waliofanyiza asilimia 2.5 ya Jeshi la India walifanya kazi tu katika maeneo yasiyo ya kivita. huku taifa jirani la Pakistan likiwa na takribani wanawake 20 marubani wa ndege za kivita. Jeshi la Pakistan lilianza kuwafunza wanawake majukumu ya vita mwaka 2006.

Comments are closed.