
Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es salaam (DART) imetangaza route mpya ya Mabasi ya mwendokasi yameanza kutoa huduma Morocco – Kawe kupitia Barabara ya Mwai Kibaki.
Hii ni njia ya tatu kwa mabasi hayo kuanza kutoa huduma kwa siku za hivi karibuni baada ya Shekilango – Mwenge (via Barabara ya Shekilango) na Morocco – Mwenge (via Barabara ya Bagamoyo).

