The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mwanajeshi wa India Aliyepotea Miaka 38 Iliyopita Wapatikana Kwenye Barafu

0
Chandrashekhar Harbola

MWILI wa mwanajeshi wa India aliyepotea miaka 38 iliyopita umepatikana kwenye mabarafu baada ya kikosi cha jeshi kufanya doria tangu wiki iliyopita katika eneo la Siachen linalotumiwa na wanajeshi kwa ajili ya kujificha, kujikinga risasi au bomu.

 

Mwanajeshi huyo amefahamika kwa jina la Chandrashekhar Harbola na kueleza kwamba miili mingine 15 ilipatikana huku askari watano hawajulikani walipo.

 

Kikosi kilichokuwa na askari 20 kilinaswa katika maporomoko ya theluji kwa kile kinachojulikana kama uwanja wa mapambano au vita uliopo sehemu za milimani, kwenye mpaka wa India na Pakistan.

 

Kikosi hicho kilipokaribia eneo la tukio wakakuta mwili ambapo wakakuta namba ya kitambulisho cha jeshi na kikosi cha Harbola, iliyochorwa kwenye kipande cha chuma.

Wazazi na ndugu na jamaa wa Chandrashekhar Harbola waliomsubiri kwa miaka 38 wakiomboleza

Aidha, kikosi hicho kilifikisha taarifa hizo makao makuu na baada ya ukaguzi wa kina wa kumbukumbu zao, walibaini kuwa mwili huo ulikuwa wa askari aliyepotea anayeitwa Chandrashekhar Harbola.

 

Umati mkubwa wa ndugu, majirani na wananchi ulikuwa umekusanyika kwa ajili ya kumpa heshima zake, tukio ambalo lilikuwa likiambatana na

nyimbo mbalimbali za huzuni ukiwemo unaosema Chandrashekhar Harbola hawezi kufa.

 

Machozi yalimtoka kila mtu aliyekuwepo eneo la tukio na wengi wao hawakuamini kwamba mwili wake ulikuwa umepatikana na kupelekwa nyumbani kwa heshima ya kijeshi.

Wanajeshi wa India wakitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Chandrashekhar Harbola

Tangu mwanajeshi huyo apotee mwaka 1984 mkewe hakutaka kuolewa kwa kuwa aliamini mumewe yupo hai na huwenda alitekwa au kuwekwa kizuizini na Wapakistan, waliokuwa wakipambana nao vitani.

 

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply