Mwinyi Zahera amuonya Chama

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, Amemuonya kiungo wa Simba, Claytous Chama raia wa Zambia, baada ya kusema kuwa, asitarajie kuwasumbua AS Vita Club ya DR Congo kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye mechi nyingine.

 

Zahera ametoa onyo hilo wakati Simba ikitarajiwa kucheza na AS Vita kwenye mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi ambapo mechi hiyo itachezwa Januari 19, mwaka huu nchini DR Congo. Kabla ya hapo, Simba itacheza na JS Saoura ya Algeria, Jumamosi hii.

 

Kocha huyo licha ya kuinoa Yanga, lakini ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo ambapo anafanya kazi na kocha Florent Ibenge ambaye ndiye kocha mkuu wa AS Vita.

 

Mcongo huyo aliyetwaa tuzo tatu za Kocha Bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu, alisema licha ya Chama kuwa na uwezo mkubwa na msaada kwa timu yake, lakini hafikirii kwamba ataisumbua AS Vita kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji wengi wazoefu waliocheza mechi nyingi za kimataifa na wachezaji wakubwa na wakawazuia.

 

“Chama ni mchezaji mzuri na anaisaidia sana Simba, lakini asifikirie kwamba anaweza kuisumbua AS Vita kama alivyofanya kwenye mechi zilizopita.

 

“Katika kikosi cha AS Vita, kuna wachezaji baadhi nimewafundisha wakiwa timu ya taifa ya DR Congo na tumekutana na timu zenye wachezaji wakubwa kama Yaya Toure, lakini wakafanya vizuri, sasa Chama anatakiwa ajipange kweli,” alisema Zahera.

 

SAID ALLY, Dar es Salaam.

ZAHERA Agoma Kumrudisha YONDANI, Amganda AJIB

Loading...

Toa comment