The House of Favourite Newspapers

MWITA ATAKA HALMASHAURI ZA DAR KUZIKA WASIO NA NDUGU

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, (mbele) akiongoza kikao  cha madiwani leo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa jiji,  Sipora Liana.
Madiwani wakifuatilia kwa umakini hoja mbalimbali zinazotolewa na wajumbe wengine.
Diwani wa Kata ya Mbagala Kibonde Maji, Abdala Mtinika,  akitoa hoja.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita,  akiongoza kikao  cha madiwani leo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa jiji,  Sipora Liana.
MSTAHIKI Meya wa  Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amezitaka halmashauri zote  katika jiji lake  kuajiri watumishi watakaozika watu ambao watabainika kuwa hawana ndugu.
Aliyasema hayo jana katika kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam  ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inapotokea na kwamba changamoto iliyopo ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“Tulikubaliana  jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndiyo wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao,” amesema Mwita.
“Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, tulikubali kuchangia usafiri, dawa na sanda,” amesema.
Amefafanua kuwa watu  wasiokuwa na ndugu wanapokufa na  kukaa hospitalini zaidi ya siku 20, jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali.

Comments are closed.