The House of Favourite Newspapers

Mziki Mzima Yanga SC Warejea Kuivaa Simba

Wachezaji wa timu ya Yanga.

KIUNGO wa Yanga, Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe amefunguka kuwa anafurahia baada ya kupona kwa jeraha lake la goti na kuweza kurejea uwanjani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Mzambia George Lwandanima.

 

Mbali na Kamusoko, pia wachezaji wengine wawili Donald Ngoma na Amissi Tambwe wanatarajiwa kurejea uwanjani hivi karibuni.

Hawa wanarejea kipindi ambacho timu yao inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakapigwa Machi 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Kwa muda mrefu Kamu­soko nyota wa zamani wa FC Platinum ya Zimbabwe alikosekana kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa nje akijiuguza jeraha hilo ambalo alilipata zaidi ya miezi minne iliyopita.

 

Hadi sasa kiungo huyo tayari amerejea ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo na tayari ameshafanikiwa kucheza michezo miwili ule wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Roll­ers ya Botswana ambapo mechi zote hizo hakufani­kiwa kumaliza dakika 90.

 

“Nilikuwa na wakati mgumu nilipokuwa ma­jeruhi kwa sababu hii ni kazi yangu, hivyo ilikuwa inaniuma kuona nipo nje, ni vizuri nimepata nafuu na nina furaha kurudi uwanjani tena,” aliandika Kamusoko kwenye Mtandao wa Instagram.

 

Wakati Kamusoko akirejea na kuanza kuitumikia Yanga kikamilifu, wachezaji Amissi Tambwe na Donald Ngoma nao hivi karibuni wanatara­jiwa kurejea tena uwanjani kuitumikia timu hiyo.

 

Kama Tambwe na Ngoma wakirejea uwanjani basi itakuwa mbaya sana kwa upande wa Simba ambao wa­likuwa wanatarajia kuvaana na Yanga ambayo haina wache­zaji wengi wenye uzoefu.

Stori: Said Ally, Dar  es Salaam

Comments are closed.