The House of Favourite Newspapers

Nafasi Za Kazi Za Maofisa Usambazaji Global Publishers

Global Publishers & General Enterprises LTD, kampuni ya ucha­pishaji wa magazeti, ina nafasi za kazi za Maofisa Usambazaji wa Magazeti katika mikoa mbalimbali nchini, wenye elimu na sifa zifuatazo:

ELIMU:

Wanahitajika vijana wa kiume na kike wenye elimu ya Chuo Kikuu wenye shahada ya kwanza ya Elimu ya Biashara.

SIFA:

Aidha, mtarajiwa awe kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 25, mwenye uzoefu wa kufanya kazi za usambazaji wa bidhaa. Wenye uzoefu wa usambazaji wa magazeti watafikiriwa kwanza.

Majukumu ya kazi yatakuwa kuangalia mahitaji ya soka na kupanga mgao kulingana na mahitaji ya soko na kisha kusimamia usambazaji wake na mwisho kuendelea kutafuta masoko mapya.

Mwisho:

Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuma barua yako ya maombi ya kazi haraka, iliyoandikwa kwa mkono wako ukiambatanisha na maelezo yako ya kikazi (CV) na nakala ya cheti/vyeti vyako, kwa:

MENEJA MKUU

S.L.P 7534

DAR ES SALAAM

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Mori (Mori Road). Simu: 0715 288627. Mwisho wa kupokea maombi ni Januari 14, 2018.

INASIKITISHA Binti Miaka 12 Aliyepooza Akaa Ndani mwaka 1 Bila Msaada

Comments are closed.