The House of Favourite Newspapers

Kichuya Ajichongea Kwa Kocha Simba

Ramadhani Kichuya.

KAMA ulidhani Ramadhani Kichuya ni staa pale Simba na kamwe hawezi kuguswa basi sahau kwani kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Masoud Djuma amesema hakuna mchezaji mwenye nafasi ya kudumu.

 

Djuma raia wa Burundi amesema; “Sina mchezaji mwenye namba ya kudumu na nitampanga mchezaji kulingana na aina ya mfumo wa uchezaji nitakaoutumia kutokana na timu nitakayokutana nayo.”

 

Kocha huyo ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Shiza Kichuya kuonekana amechukizwa na kitendo cha kutolewa nje kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Azam FC kwenye Kombe la Mapinduzi.

 

Kichuya mara baada ya kufanyiwa mabadiliko inaelezwa alisusia kukaa katika benchi la timu hiyo na kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia kabla ya Djuma kumtetea kuwa alimruhusu kwenda jukwaani.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Djuma alisema amekuja na mfumo tofauti ambao unawaruhusu wachezaji wote kucheza katika timu yake kama alivyofanya kwenye Kombe la Mapinduzi.

 

Akithibitisha hilo, Djuma alisema kiungo mshambuliaji, Nicholas Gyan hakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini alimtumia kama beki wa kulia.

 

“Timu yangu aina mchezaji mmoja tegemeo au mwenye namba ya kudumu katika timu, mimi ninapanga timu kutokana na mfumo nitakaoutumia kulingana na aina timu ninayokutana nayo.

 

“Kumtoa Kichuya katika mechi na Azam ilikuwa ni mipango yangu katika kubadili mfumo ili aingie mchezaji mwingine atakayemudu aina ya uchezaji niliyokuwa nitaka icheze ili tupate ushindi.

 

“Kila mchezaji katika kikosi changu ana nafasi ya kucheza kwani mifumo na aina yangu ya uchezaji ambayo ninataka wachezaji wangu wacheze inawaruhusu wachezaji wote kucheza,” alisema Djuma.

Simba Kwisha Kazi Mapinduzi Cup

Comments are closed.