The House of Favourite Newspapers

NAFASI ZA KAZI: MKUU WA USAMBAZAJI WA MAGAZETI

Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises LTD, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, ina nafasi za kazi za Maofisa Usambazaji wa Magazeti katika mikoa mbalimbali nchini, wenye elimu na sifa zifuatazo;

 

Anahitajika kijana wa kiume mwenye umri wa miaka isiyozidi 35 na elimu ya chuo kikuu, anayejua kuendesha pikipiki na gari ambaye ana uzoefu wa kufanya kazi ya usambazaji wa magazeti wa muda mrefu.

 

Majukumu ya kazi yatakuwa kusimamia upangaji wa mgao wa magazeti kulingana na mahitaji ya soko kisha kusimamia usambazaji wake na mwisho kuendelea kutafuta masoko mapya.

 

Mwisho:

Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuma barua yako ya maombi ya kazi haraka iliyoandikwa kwa mkono wako ukiambatanisha na maelezo yako ya kikazi (CV) na nakala ya cheti/vyeti vyako kwenda kwa;

MENEJA MKUU

S.L.P 7534

DAR ES SALAAM

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu,

Sinza-Mori (Mori Road). Simu: 0715 288627

Mwisho wa kupokea maombi ni

Oktoba 10, 2018.

Comments are closed.