The House of Favourite Newspapers

Nahodha Yanga SC awalilia Kessy, Chirwa

NAHODHA msaidizi wa timu ya Yanga Juma Abdul amesema kuwa kuondoka kwa wachezaji waliokuwa wakianza kikosi cha kwanza ndani ya timu hiyo kumeiyumbisha timu hiyo hali ambayo itachukua muda kuweza kujipanga.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Abdul alisema kuwa timu inaundwa na wachezaji na kuondoka kwa mmoja ama wawili kunasababisha kuyumba kwa timu hivyo kazi kubwa inabaki kwa mwalimu kuandaa kikosi upya.

 

“Wachezaji wetu kama Hassan Kessy pamoja na Chirwa ambao wameondoka ndani ya timu tunawakumbuka sana kwa kuwa tayari tulikuwa tumetengeneza muunganiko mzuri ambao ulikuwa unaleta ushindani uwanjani.

 

“Kwa sasa kazi kubwa ya kutengeneza kikosi ipo chini ya mwalimu kwa kuwa yeye ndiye anayejua nani ataziba nafasi za wachezaji ambao wameondoka, hivyo matumaini yangu ni kwamba timu itasimama na itafanya vizuri katika mashindano itakayoshiriki lakini hilo halizuii kusema kuwa wameacha pengo,” alisema Abdul.

 

Chirwa ambaye alikuwa staa wa Yanga kwa msimu uliopita amesajiliwa na Ismailia ya Misri huku Kessy ambaye mkataba wake umemalizika na amejiungana Nkana Red Devils FC ya nchini Zambia kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Lunyamadzo Mlyuka,

Dar es Salaam

Comments are closed.