The House of Favourite Newspapers

NAIBU WAZIRI KILIMO ATEMBELEA MAGHALA YA KOROSHO PWANI

Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba (wa pili kushoto) akiwa ndani ya ghala la korosho.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba (wa kwanza kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa kiongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani, Rajab Ngonoma (katikati).
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba (wa kwanza kushoto) akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani juu ya namna zoezi linavyoendelea la ukusanyaji korosho.

Mgumba akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika wa Mkoa wa Pwani. 

 

Naibu Waziri  wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba jana amefanya ziara ya kikazi katika wilaya tatu za Mkoa wa Pwani za Kibaha, Mkuranga na Kibiti kwa lengo la kukagua jinsi zoezi la ukusanyaji wa korosho katika maghala ya vyama vya ushirika linavyoendelea.

 

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara hiyo ya kikazi, Mgumba alisema lengo kubwa lilikuwa ni kutembelea maghala makuu ya vyama vya ushirika yanayotumika kuhifadhia korosho ili kujionea mwenendo wa ukusanyaji korosho unavyoendelea.

 

Akiwa katika ziara hiyo, Mgumba amewahakikishia wakulima kwamba wote watalipwa fedha zao kama alivyoagiza Rais Dk. John Pombe Magufuli na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha uhakiki unafanyika kwanza kabla ya wakulima kuanza kulipwa.

 

“Serikali ya Rais Magufuli ipo pamoja na wakulima kuhakikisha hawanyonywi na walanguzi, nawahakikishia kwamba baada ya uhakiki kukamilika, kila mkulima atalipwa fedha zake zote mara moja. Hakuna mkulima atakayekopwa hata mmoja,” alisema Mgumba.

Comments are closed.