The House of Favourite Newspapers

NAY wa Mitego Agawa Pesa kwa Mama Ntilie Manzese – Video

MWANAMJUZIKI wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ametinga sokoni Manzese jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, na kugawa pesa kwa wakinamama wanaofanya biashara ndogondogo za kuuza chakula maarufu kama mama ntilie.

 

Mbali na kugawa pesa, Nay pia amesikiliza changamoto zinazowakabili akinamama hao na kutoa ahadi ya kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau wa maendeleo watakaoweza kuchangia ili wakinamama hao waweze kufanya shughuli zao vizuri.

 

Ikumbukwe kuwa, Nay wa Mitego amezaliwa na kukulia eneo hilo la Manzese, hivyo anachokifanya ni kurudisha fadhila kwa wakazi wa eneo hilo na kuwakwamua akina mama wenye biashara hizo ndogondogo ili siku moja wafikie malengo yao.

VIDEO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.