The House of Favourite Newspapers

Nchi Zenye Watu Wanene Zaidi Duniani kwa Mwaka 2018

1 – Kuwait – Asilimia 42.8% ya watu wake ni wanene.

Kwa mujibu wa orodha ya mwaka huu — 2018 — Kuwait inaongoza duniani kwa kuwa na watu wengi zaidi wanene duniani kutokana na kula mno aina mbalimbali za vyakula na kutofanya mazoezi.  Hivi sasa duniani, asilimia 13 ya walimwengu ni wanene, wenye vitambi au wenye uzito mkubwa.

2 – Saudi Arabia – 35.2%

Nchi hii ni ya pili kwa kuwa na watu wanene duniani ambapo tatizo hilo linachukua theluthi moja ya wanawake nchini humo, tatizo linalotokana na kula vyakula mbalimbali kupita kiasi na kutofanya mazoezi.

3 – Egypt (Misri)– 34.6%

Kuenea kwa viwanda nchini humo na kupatikana kwa chakula kwa bei ya chini, kumesababisha watu wengi kunenepa, ambapo waliokumbwa na tatizo hilo hasa ni wakazi wa mijini kuliko wanaoishi sehemu za mashambani.

4 – Jordan – 34.3%

Kama zilizo nchi nyingine za Arabuni, Jordan nayo imo katika orodha ya watu waliokumbwa na unene, hususani wanawake ambao, kwa mila za Kiarabu, akishaolewa anakuwa ni mtu wa kukaa nyumbani na kula tu, hivyo kuongezeka uzito.

5– United Arab Emirates (Falme za Kiarabu) – 33.7%

Hizo zikiwa ni nchi za Arabuni na zenye utajiri mkubwa wa mafuta, chakula hupatikana kwa bei ya chini, hivyo kuwafanya wananchi kuvimudu  kirahisi — matokeo yake ni kunenepena.

6 – South Africa – 33.5%

Afrika Kusini imeingia katika orodha hii kwa mara ya kwanza, kitu ambacho ni cha ajabu, kwani nchi nyingi za Afrika ziko katika umaskini na chakula ni cha tabu.  Hata hivyo katika nchi nyingi zinazokumbwa na njaa, bado kuna watu wanene, na Afrika Kusini ni mojawapo.

Comments are closed.