The House of Favourite Newspapers

NDANDA FC YAIBANA MBAVU YANGA SC – VIDEO YA MABAO IKO HAPA

Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mabingwa wa kihistoria Yanga kulazimishwa suluhu ya bao 1-1 na Ndanda FC. Yanga walikuwa wa kwanza kufungwa na Ndanda kupitia Nassor Hashim mnamo dakika ya 16 tu ya mchezo.

 

Yanga nao walifanikiwa kujibu mapigo kwa kusawazisha kupitia mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajibu ambao ulimfika Japhary Mohammed na kuumalizia kwa njia ya kichwa ikiwa ni dakika ya 24.

 

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 26 sawa na Simba ikiwa imecheza michezo 10. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 1-1 Ndanda FC.

TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.