The House of Favourite Newspapers

Ndege Ya Boeing 787-8 Dreamliner Ilivyopokelewa (Picha + Video)

Rais Magufuli akitoa hotuba kabla ya ndege kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu akisalimia baada ya kufika uwanjani hapo.
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania ikitua katika ardhi ya Tanzania kwa mara ya kwanza.
Ndege hiyo ikitafuta sehemu ya kusimama.
Ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya kupokelewa.
Marubaini na viongozi mbalimbali walioileta ndege hiyo wakishuka muda mfupi baada ya ndege kutua.
Rais Magufuli akiongea jambo na viongozi wa serikali akiwa ndani ya ndege hiyo.

 

RAIS Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 amewaongoza Watanzania kuipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania. Viongozi mbalimbali wameungana na rais kuipokea ndege hiyo.

(PICHA: RICHARD BUKOS | GPL)

Comments are closed.