The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Magufuli Yakabidhiwa Kwa ATCL

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (wa pili kushoto) akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Injinia Emmanuel Korosso.

SERIKALi imekabidhi ndege yake aina ya Fokker 50 kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais John  Magufuli.

Hafla fupi ya kukabidhi ndege hiyo imefanyika leo, Aprili 1, 2019,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Fokker 50 ilikuwa ikibeba viongozi mbalimbali lakini Rais Magufuli aliagiza ikabidhiwe kwa ATCL ili kuongeza nguvu na kuendelea kulikuza shirika hilo ambalo amedhamiria kuliboresha.

 

Comments are closed.