The House of Favourite Newspapers

NDOA YA KIM, KANYE MGUU NJE MGUU NDANI !

Related image

INAPUMULIA mashine! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kitumbua kuingia mchanga katika ndoa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim kardashian kisa kikidaiwa ni kuposti picha za utupu bila kujali ni mama wa watoto watatu.

Ishu nzima ilianza kubumburuka, katika ‘episode’ ya mwisho ya kipindi chao cha ‘Keeping Up With The Kardashians’ ambapo, Kim alikuwa anazungumza na dada yake ambaye ni Kourtney Kardashian akimuelezea chanzo cha ugomvi wake na mumewe (Kanye West) ulianza baada ya kumwambia kuwa hana haki ya kumpangia cha

kupost katika mtandao wake wa kijamii.

Watu wengi mitandaoni walisema, Kim anatafuta sababu ya kuachana na Kanye kwa sababu inabidi aheshimu kuwa jamaa huyo ni mume wake na asikilize anachomwambia.

Comments are closed.