The House of Favourite Newspapers

Njemba Apewa Kichapo Moro Kwa ‘Kuwasachi’ Wananchi Mifukoni

KIJANA  mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja juzi alinusurika kifo baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wananchi eneo la Kihonda ambako walifika kumshuhudia kiboko aliyekuwa amevamia eneo hilo na hatimaye kuuawa na maofisa wanyama.

Mtu huyo anadaiwa kutumia fufsa hiyo ya msongamano wa watu kuwasachi mifukoni na kuwaibia simu na pesa.

Katika kuwasachi watu, kijana huyo alimpapasa mtu mmoja ambaye aligundua hila yake kisha kumwitia “mwizi” ambapo watu waliacha kumshangalia kiboko na kuanza kumshambulia.

 

Katika hali ya kushangaza, kijana huyo aliamua kukimbilia kwa mwandishi wetu aliyekuwa akipiga picha na kuomba amsaidie asipigwe na wananchi hao.

“Shekidele nisaidie mimi sio mwizi wananisingizia!”alisema kijana huyo akimwambia mwandishi wetu japokuwa yeye (mwandishi) hamfahamu.

 

Hata hivy0, wananchi waliendelea kumpa kipigo hadi alipookolewa na polisi.

Na Dunstan Shekidele, Morogoro

Comments are closed.