The House of Favourite Newspapers

Njia Tano Za Kumtambua Mwanamke Kicheche/Hajatulia

 

Waliosema mapenzi yana run dunia hawakukosea kwani wamesema jambo ambalo ni asilimia 100 ukweli kutokana na uchunguzi wao na kila mtu anahitaji mwenza ili akamilike.

Wanaume/wavulana wengi sana wanapenda baadhi ya wasichana/wanawake ambao watafurahi nao kimapenzi lakini kati yao huwa wanatokea kuumizwa na kulizwa baada ya kutambua kuwa aliyempenda sio ambaye alitegemea.

Hilo huletwa na ukosefu wa elimu ya mahusiano ambayo itakuwezesha kuwajua baadhi ya waschana na tabia zao.

Kuanzia leo baada ya kujua mambo/njia tano muhimu za kumtambua mwanamke/mschana  kicheche/hajatulia utakuwa mwisho wa kulizwa na kama ulikuwa unataka kufanya uchaguzi wa mke bora, basi itakuwa faida kwako.

1. Siyo rahisi kupenda

Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu, mara nyingine hushindwa kuongea lolote na utaweza kutambua kwenye matendo yake.

2. Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha

Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa siku zote kuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

3. Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote

Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka. Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

4. Anamarafiki wakiume kwa manufaa

Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale. Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.

5. Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka

Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake. Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.

CARINA BADO USAHA UNATOKA TUMBONI, HAAMINI HADI LEO YUPO HAI, ANATUMIA ELFU 60 KILA SIKU KUSAFISHWA

Comments are closed.