The House of Favourite Newspapers

NMB Yazindua Huduma Mpya ya Masta Boda

Dunia inakwenda kwa kasi sana! Kutokana na changamoto ya foleni hasa katika maeneo ya mijini, watu wengi siku hizi hupendelea zaidi usafiri wa bodaboda!

Watumiaji wa bodaboda wameongezeka maradufu lakini pia, vijana wanaotoa huduma ya usafiri wa bodaboda wameongezeka maradufu na kutoa ajira kwa Watanzania wengi.

 

Sasa habari njema kwa watumiaji na waendeshaji wa bodaboda, mijini na vijijini ni kwamba benki ya NMB imezindua huduma mpya iliyopewa jina la Masta Boda ambapo mteja mwenye akaunti kupitia NMB Bank, anaweza kufanya malipo kwa urahisi kabisa, papo hapo!.

Kwa wewe dereva wa bodaboda, ili uweze kuwa na uwezo wa kupokea malipo kwa njia hiyo, unapaswa kufuata hatua zifuatazo.

 

Unatakiwa kuwa na account ya NMB ambapo baada ya kufungua akaunti utapewa QR Code ambayo imewekwa kwenye ‘reflector jacket’, jaketi maalum ambalo huvaliwa na waendesha bodaboda waliosajiliwa kutoa huduma hiyo.

 

Faida anayoweza kuipata dereva wa bodaboda aliyejiunga na huduma hii, ni kwamba mauzo yataongezeka maradufu kutokana kuongezeka kwa wigo wa wateja wa benki zote zenye ‘app’ na pia wateja wanaotumia huduma za kifedha kutoka mitandao ya simu.

 

Unapotumia huduma hii, huna haja ya kuwa na wasiwasi na chenji kwa wateja wako, mfumo wa kukurahisishia fedha zako zote kuwekwa kwenye akaunti yako husika bila ya wewe kwenda benki.

Pia, mfumo huu unahakikisha usalama wa fedha zako kwa sababu fedha zinaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki na si rahisi kupoteza fedha zako kwa namna yoyote ile.

 

Kwa dereva wa bodaboda mwenye malengo, mfumo huu husaidia kufuatilia mpangilio wa fedha zako na kiasi unachoingiza kwa siku bila kuwa na mianya ya matumizi mabaya ya fedha na hivyo kukurahisishia kutimiza malengo yako.

 

 QR code ni mfumo wa malipo wenye muonekano wa ‘bar code’ ambao unatumia jina la mfanyabiashara kupokea malipo. Ni mfumo rahisi kuliko ule wa USSD unaotumika katika simu za kawaida na huhitaji kuingiza namba nyingi bali mteja anapiga picha na kuainisha muamala kwa kuingiza namba za siri.

 

Unapojiunga na huduma hii, wateja watajua kwamba unapokea malipo kwa QR Code kutokana na jaketi la njano lenye reflector yenye picha ya visa au MasterCard pamoja na barcode ambayo wateja watalazimika kutumia kufanya malipo.

 

Namna ya kutumia huduma hii, mteja anatakiwa kufanya mambo yafuatayo:

  1. Piga *150*66# kisha ingiza PIN yako ya NMB Mobile.
  2. Chagua huduma za malipo.
  3. Chagua Scan to Pay.
  4. Kisha Chagua Visa au Master Pass.
  5. Ingiza namba ya mwenye QR Code.
  6. Mteja atatakiwa kuingiza PIN yake ya NMB Mobile kuthibitisha muamala.
  7. Baada ya hapo muamala utakuwa umekamilika; mteja na mwenye QR code wote watapata meseji kwamba muamala umekamilika.

 

Kwa wateja wengine wasio wa NMB, nao wanatakiwa kufuata taratibu kama za hapo juu, japo kunakuwa na tofauti kidogo.

  1. Ingia kwenye app ya Benki yako.
  2. Chagua scan to pay.
  3. Piga picha QR Code mbele yako.
  4. Ingiza kiasi unacholipia.
  5. Ingiza PIN ya Benki yako husika.
  6. Utapokea meseji ya uthibitisho wa muamala wako.

 

Ili kujua kama akaunti yako imeingiziwa fedha kutoka kwa mteja, utatumiwa meseji papo hapo kuonesha kufanikiwa kwa muamala wako. Meseji isipoingia, unaweza ukapata nakala fupi ya miamala yako papo hapo kwenye NMB Mobile.

WEBSITE ===> NMB Bank Plc – Official Site

FACEBOOK ===> OfficialNMBTZ

INSTAGRAM ===> nmbtanzania

Comments are closed.