The House of Favourite Newspapers

MADAI YA KUOLEWA NA ZITTO, OFM YAMFUNGIA KAZI MKE WA FILIKUNJOMBE

DAR ES SALAAM: Kilinuka wiki iliyopita mitaani kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amejisogezea jiko jingine kwa kumuoa mke wa marehemu Deo Filikunjombe (Mbunge wa zamani wa Ludewa, Njombe), Sarah watu wakasema: “Ohooo, yamekuwa hayo tena!”  

 

Chanzo cha habari ni gazeti moja la kila siku hapa nchini ambalo Septemba 10, mwaka huu liliandika kwenye ukurasa wake wa mbele: “Zitto adaiwa kuoa mke wa Filikunjombe.”

Vishereheshi vya habari hiyo vilisomeka: “Amhamisha Kijichi, ampangishia nyumba Masaki, mazito yabainika.” Habari ambayo ukweli wake Amani halijauthibitisha. Baada ya gazeti hilo kusomeka hivyo gumzo likatawala kwenye mitandao ya kijamii na hoja zikawa; vipi Zitto amuoe mke wa swahiba wake aliyetangulia mbele za haki au ndiyo wasemavyo waswahili kizuri kula na ndugu? Wengi hawakuamini habari hiyo.

AMANI MZIGONI

Mambo yalivyozidi kuwa mengi huku kila mtu akieleza yake; Amani likaona ni vyema kutuma kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kufanya uchunguzi ili kujua ukweli wa jambo hilo.

 

“Habari hii imeshtua sana, fanyeni uchunguzi ili muwaondolee watu maswali, maana kuna wengine wanaamini na wengine hawaamini yaliyoandikwa na gazeti hilo,” alisema kiongozi wa OFM akiwaelekeza vijana wake kuanza kazi ya uchunguzi. Aidha, yalipotolewa maelekezo hayo, OFM walianza kufanya uchunguzi wao kwa kuchimbua ukweli wa mjane huyo kupangishiwa na Zitto nyumba Masaki jijini Dar es Salaam. Majibu ya awali hayakuweza kutoa ‘doti’ zozote zinazounga kuwepo kwa nyumba hiyo ambayo amehamia Sarah, kutoka Kijichi alipokuwa akiishi na marehemu mumewe.

Image result for sarah filikunjombe

“Hamna bwana, Sarah angehamia huku mimi kama rafiki yake ningejua. Mimi hanifichi kitu Sarah,” alisema rafiki mkubwa wa Sarah aliyeomba hifadhi ya jina. Mbali na mtu huyo wa karibu, OFM ilizungumza na marafiki mbalimbali wa Sarah ambao walitilia shaka uwezekano wa Sarah kuolewa na Zitto kisha kupangishiwa nyumba Masaki.

 

OFM WAIBUKA KIJICHI

Baada ya kutoambulia chochote Masaki, OFM walihamishia majeshi katika nyumba ya Mtoni Kijichi lengo ni kujua kama ni kweli kahama au bado anaishi hapo.

OFM wakiwa mita kadhaa kutoka nyumbani kwa Sarah walikutana na kijana mrefu mweupe ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake na kuanza mazungumzo naye:

OFM: Eee bwana eee, samahani wewe mwenyeji mitaa hii.

KIJANA: Yaaa ni mwenyeji.

OFM: Sisi wageni kidogo; hivi nyumba ya marehemu Filikunjombe iko wapi hapa? (wanazuga kuuliza)

KIJANA: Si hiyo hapo mbele.

OFM: Lakini mke wa Filikunjombe si hakai hapa siku hizi?

KIJANA: Kwa nini? Leo tu nimemuona,” alijibu kijana huyo na kuwafanya makamanda wa OFM kuielekea nyumba hiyo.

WAKUTA MAGARI KIBAO YA KIFAHARI

Makamanda wa OFM walipokita rada katika nyumba hiyo, walishuhudia magari kibao ya kifahari ndani ya nyumba hiyo huku kukionekana kuna utulivu.

WABISHA HODI

Kikosi kazi cha OFM kilitawanyika katika kona mbalimbali za nyumba hiyo huku makamanda wawili wakienda kubisha hodi kujiridhisha.

Makamanda hao walipofika getini, kwa mbali walimuona Sarah akiwa amekaa na watu kadhaa ambao baadhi yao OFM iliwafahamu kama ndugu wa marehemu Deo. “Sarah hayupo,” alisikika kijana huyo aliyekuja kukutana na OFM getini.

OFM: Sisi tuna shida naye (Sara) mfuate tu pale, si yule tunamuona na yeye anatujua sisi hana neno; kamwambie.

KIJANA: Hayupo nimewaambia.” Kijana huyo aliendelea kukataa uwepo wa Sarah jambo lililowalazimu OFM kujieleza zaidi ili kuondoa hali ya wasiwasi iliyokuwepo kwa kijana huyo.

Baada ya dakika kadhaa ya majadiliano, kijana huyo alikwenda katika kikao alichokuwepo Sarah na kumueleza kuhusu ujio wa OFM. “Kawaambie, siwezi kuzungumza nao lolote,” Sarah alimtuma yule kijana arudi tena kwa makamanda wa OFM waliokuwa bado wamezuiliwa getini wakisubiri hatma ya kuzama ndani.

Kwa kuwa makamanda walikuwa wakisikia na kumuona Sarah jinsi alivyoonekana kutokuwa kwenye hali nzuri, walisubiri tu kusikia kauli ya kijana huyo licha ya kuwa wameshasikia kila kitu. “Amesema hawezi kuongea chochote. Hayupo kwenye hali nzuri amesema mumuache,” alisema kijana huyo.Image result for Cyprian Musiba

MBINU ZAGEUZWA

“Sikia, sisi ni watu wema tu (wakajitambulisha majina) na tumetokea Global Publishers, kiongozi wetu anatambua uwepo wetu na lengo jema tu kwake.

“Tunataka kujua kauli yake kuhusu madai ya yeye kuolewa na Zitto nadhani hata wewe umezisikia hizi habari,” mmoja wa makamanda hao akamueleza yule kijana. “Ok, ngoja nikamueleze kama kiongozi wenu anajua uwepo wenu hapa nimsikie atasemaje,” alijibu kijana huyo huku akiimarisha ulinzi wa nyumba hiyo kwa kufunga geti vizuri kwa ndani.

MAJADILIANO YAENDELEA

Alipofika yule kijana na kumueleza Sarah kwamba vijana hao wametokea Global, alichukua simu yake na kumpigia mmoja wa viongozi wa Global. “Eeeh eti umetuma watu wako hapa? (anawataja majina),” alisikika kwa mbali Sara akizungumza na mmoja kiongozi wa Global.

SIMU YA SARAH YALETWA KWA MAKAMANDA

Baada ya mazungumzo mafupi ya Sarah na kiongozi huyo, yule kijana alipewa simu na Sarah aje kuwapa makanda wa OFM.

OFM: Ndiyo kiongozi nakupata…

KIONGOZI: Nilikuwa sina habari kumbe mmeshafika huko?

OFM: Ndiyo mkuu tulikuwa tunataka kujua ukweli wa haya madai ya mke wa Deo na Zitto…

KIONGOZI: Anyway, huyo mama amenieleza kuwa hayuko vizuri kwa sasa hebu mpeni simu niongee naye.

SIMU YAREJESHWA KWA SARAH

Sarah alirudishiwa simu na kuzungumza kwa muda kisha yule kijana akarudi tena kutoa majibu kwa makamanda kwamba wanaomba aachwe kwa muda kwa kuwa hayuko sawa na kwamba wapo katika kuchukua hatua juu ya habari hiyo. “Kwani kikao hicho cha familia humo ndani kinahusu suala hili la habari ya Sarah na Zitto?” Amani lilimchimba yule kijana ambaye alieleza mengi ambayo hata hivyo, aliomba yasiandikwe, jambo ambalo OFM wamelizingatia.

Baada ya kuelezwa mengi OFM ilianua jamvi eneo hilo huku ikiwa tayari imejiridhisha kwamba Sarah anaishi hapo, hajawahi kuhama na hata majirani mbalimbali waliohojiwa walisema mjane yupo hapo tangu Deo alipofariki dunia Oktoba 16, 2015 kwa ajali ya helikopta kipindi cha kuelekea kampeni za Uchaguzi Mkuu.Image result for zitto kabwe

MKURUGENZI, ZITTO HAPATOSHI

Wakati huohuo, baada ya madai hayo ya kuwepo kwa ndoa ya Zitto na Sarah kuibuliwa na gazeti hilo (jina kapuni) majibizano mitandaoni baina ya Mkurugenzi wa gazeti aitwaye Cyprian Musiba na Zitto yaliibuka.

Zitto aliandika hisia zake kuhusu habari hiyo kupitia mtandao wake wa Facebook na kumtaka mkurugenzi huyo athibitishe au akanushe madai hayo na akishindwa kufanya hivyo ndani ya siku moja basi familia yake Musiba isimlaumu (Zitto) kwa hatua atakazochukua.

MUSIBA AJIBU MAPIGO

Kufuatia ujumbe huo wa Zitto ambao haukuonesha dhahiri kwamba atachukua hatua gani, Musiba alikuja na bomu kubwa kumshambuliwa Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini na kudai kuwa haogopi vitisho. “Mimi siogopi kufa. Kama ni mchawi basi aroge awe rais…” alisikika Musiba katika mahojiano yake yaliyorushwa mtandaoni.

Hadi Amani linakwenda mtamboni siku moja aliyotoa Zitto ilikuwa imemalizika bila kuwepo kwa tukio jipya, lakini rafiki wa Zitto aliliambia dawati letu kuwa mbunge huyo ana mpango wa kukifikisha chombo hicho cha babari kwenye vyombo vya sheria. Hata hivyo Zitto alipotafutwa na Amani ili lau kusikia kauli yake kuhusu sakata hili hakupatikana.

Comments are closed.