The House of Favourite Newspapers

P Funk Afichua Siri Ngoma za Zamani Kuishi!

P Funk ‘Majani’

MKALI wa midundo kutoka Bongo Records, P Funk ‘Majani’ amesema siri kubwa ya wasanii wa zamani ngoma zao kudumu sokoni kuliko wa sasa ni kutokana na wasanii wa zamani kufanya muziki kwa upendo mkubwa.

 

P Funk alisema, wasanii wa zamani walikuwa na moyo wa kujituma, walikuwa wanafanya muziki kutoka moyoni na walikuwa wanasota sana kuyahangaikia mafanikio.

“Wasanii walikuwa wanatoka mbali kusaka studio, walikuwa wanahaso sana kupiga kwenye kumbi ndogondogo, walikuwa wanahangaika hadi kutoka na ndiyo maana walikuwa wakifanikiwa kutoka na kweli ngoma zao zinaishi,” alisema P Funk.

 

P Funk alisema wasanii hao walikuwa wanafanya muziki si kwa kutanguliza fedha mbele, walikuwa wanafanya muziki kwa sababu walikuwa na mapenzi ya dhati na muziki.

Alipoulizwa kama ana mpango wowote wa kufanya kazi ya pamoja na wasanii wake wa zamani, P Funk alisema kwa sasa amejikita zaidi kufanya kazi na vijana wapya.

Comments are closed.