The House of Favourite Newspapers

Penny Afungukia Kilichompoteza

BAADA ya kimya cha muda mrefu, mtangazaji wa Televisheni ya Magic Swahili, Penniel MungilwaPenny’ ameibuka na kuanika sababu iliyomfanya apotee kuwa ni baada ya kuamua kujificha machoni kwa watu ili kuepukana na maneno na kujadiliwa bila sababu.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Penny alisema kuna kipindi alikuwa gumzo sana midomoni mwa watu kila kukicha ambapo aliamua kujificha ili wamsahau na kweli alifanikiwa na hiyo ilimsaidia kufanya mambo yake mengine ya maendeleo zaidi.

 

“Unajua kuna wakati watu wanaweza kukuzungumzia mpaka ukaogopa kabisa kukatiza mitaani na ndiyo iliyonitokea nikaamua kujificha na kuachana na maisha ya kujiachia klabu au sehemu za starehe, hii imenisaidia kwani wamenisahau na siku hizi wanajadili mambo mengine,” alisema Penny.

Stori: Imelda Mtema.

Daimond, Rayvanny watuma salamu nzito Basata!!

Comments are closed.