The House of Favourite Newspapers

Peter Msechu Afungukia Kufulia Kimuziki

Peter Msechu

Peter Msechu, aliyewahi kufanya vizuri na ngoma nyingi zikiwemo Relax, Mama aliomshirikisha Banana Zorro pamoja na Hasira Hasara, amefunguka kwamba hawezi kufulia kama ambavyo watu wanadai mitandaoni kwani muziki upo ndani yake na kwa sasa ameamua kutulia ili kuimarisha masuala yake ya ujasiliamali.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Msechu alisema, kwa sasa anaimarisha shughuli zake za ujasiriamali ambazo zinamuingizia kipato kikubwa cha kuandaa sherehe, kupamba maharusi na shughuli mbalimbali za kijamii.

“Ninawezaje kufulia kimuziki? Kwa watu wanaonifuatilia wataona pia nimefanya kava ya Wimbo wa Sitabaki Nilivyo. Hiyo inaonyesha kwamba bado nipo na uwezo wangu ni mkubwa. Ila nimeamua kidogo kuimarisha kwanza masuala yangu ya ujasiriamali tu,” alisema Msechu.

Boniphace Ngumije

Comments are closed.