The House of Favourite Newspapers

Polepole: Unakwenda na Gunia la Nyuki, Bastola Kwenye Kituo? – Video

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Mwaka huu kiaanza kutoa mafunzo ya ufundi stadi bure kwa vijana kuanzia wenye umri wa miaka 18 hadi 35 na kwale ambao hawatataka kuendelea na masomo ya kidato cha tano utasoma ufundi bure.

 

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi ndogo za CCm zilizopo, Lumumba jijini dar na kutoa tasmini ya uchaguzi mdogo uliyofanyika juzi.

 

“Kila mwaka tunatoa pesa kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana, katika mwaka huu wa fedha; Ilala tunatoa Tsh. 4b, Kinondoni Tsh. 5b, Ubungo Tsh. 2b, Temeke na Kigamboni kwa pamoja ni takribani Tsh. 2b kwa pamoja. Watu wanaona mambo haya.

Akizungumzia uchaguzi huo ambao CCM iliibuka na ushindi kwenye majimbo yote mawili ya Monduli Arusha na Ukonga Dar es Salaam, Polepole amesema;

 

“Wakishinda wao huwa ni uchaguzi huru na wa haki, na tume ni nzuri mno, mbona walishinda Udiwani Mbeya wakakubali, walishinda udiwani Manyara walisaini? Mtu akitoka Chadema akajiunga CCM anakuwa mtu mbaya sana, akitoka Chadema kwenda CCM ameona ukombozi.

 

“Mbona hawasemi, Uyole pale (Mbeya) wanachama na viongozi wa wamekamatwa na bastola kwenye kituo cha kupiga kura kinyume na sheria? Mwingine kaenda kwenye kituo cha kupiga kura na gunia la nyuki ili afanye nini? Alikwenda kurina asali? Huo ndo uchaguzi huru na wa haki?” alisema Polepole.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.