The House of Favourite Newspapers

Polisi Wakatisha Raha Coco Beach

   coco-beachUmati wa watu walikowa kwenye Ufukwe za Cocco.

Vibaka, Mateja wahatarisha usalama, kamari, karata tatu, machangu tishio.

Richard Bukos na Issa Mnally

DAR ES SALAAM: Polisi waliovalia sare za jeshi hilo na wengine kiraia jana, Jumapili walilazimika kuwatoa kwenye maji watu mbalimbali waliokuwa wakila raha kwenye ya Ufukwe wa Coco jijini hapa kwa ajili ya kuhofia vitendo vya uvunjifu wa amani.

Katika ufukwe huo licha ya burudani zilizokuwa zikiendelea lakini utitiri wa vibaka uliokuwa na kazi ya kuiba nguo, viatu na vitu vingine vya waliokuwa wakiogelea na kuviweka kando.

coco-beach-krismasi-4Hali hiyo ilisababisha vilio kwa baadhi ya watu hasa watoto na kinamama ambao walijikuta wakitoka kwenye maji na kukuta nguo zao zimeshaibwa na vibaka hao.

Vijana wengine wanaohisiwa kuwa watumia madawa ya kulevya ‘mateja’ walioonekana na sura zao na kukata tamaa wakiwapiga chabo kiupandeupande watu waliokuwa na vitu vya thamani.

Mateja hao wengine walionekana kuzidiwa na unga na kuangusha gari mchangani ‘kulala’ bila kujitambua ingawa wengine waliokutwa na hali hiyo hawakuwa mateja.

coco-beach-krismasi-3Wakati burudani hizo zikiendelea wajanja wa mjini nao walikuwepo na wajinga waliwao walikuwepo ambapo baadhi ya watu hasa kina mama walionekana kucheza mchezo wa karata tatu uliokuwa ukichezeshwa na makundi ya wahuni.

Mchezo ulisababisha watu kadhaa kulia baada ya kugundua kuwa wameshaibiwa.

Wengi walioibiwa hawakupewa pole bali walichekwa kwa ujinga wao wa kutapeliwa kwa wizi huo kizamani ambao umeendelea kuwaliza wajinga wasioisha hapa mjini.

coco-beach-krismasi-2Polisi akiwaondoa watu baharini baada ya muda kuisha.

Kama msemo usemao penye wengi pana mengi na ndipo penye riziki, kundi la machangudoa nalo lilitumia mwanya huo kuwanasa wanaume wakware kwa kujifanya wakiogelea na nguo za ndani ambazo sio zile za ogeleaji wao wakitumia kufuri nyepesi za kuvalia ndani.

Machangu hao walikuwa wakiogelea na kufuri hizo ambapo zilipolowana kila kitu kilionekana wazi bila uficho na hivyo kuwafanya wanaume wakware kutokwa na udenda na kushindwa kujizuia.

coco-beach-krismasi-1Njemba akiwa ‘amezima’.

Wadada kadhaa walionekana kuwanaswa wanaume kwa mtindo huo na kasha kutoka kwenye maji na kuondoka nao baada ya muda walirudi na kuendelea kuwanasa wengine kwa staili ya nenda rudi.

Wakati yote hayo yakiendelea jua lilipozama ndipo maafande hao waliamua kukatisha burudani zilizokuwa zikiendelea kwenye maji nja kuwataka watu wote watoke nchi kavu na wapandishe juu kabisa.

Baadhi wa watu walionekana kutaka kuwagomea polisi hao mpaka walipoanza kuwatoa kinguvu kwa kuwachapa bakora na kuwatishia mbwa.

Comments are closed.