The House of Favourite Newspapers

Polisi Yaua Majambazi 2 Mwanza

bundukiMWANZA: JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakati wakijaribu kutoroka.

Imeelezwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya watu hao kujaribu kuwatoroka askari polisi wakati wakiwapeleka mahali ambapo majambazi wenzao walikuwa wamejificha ili baadaye waweze kufanya uvamizi.

Jeshi la polisi mkoani humo pia limefanikiwa kukamata bunduki moja aina ya shortgun ikiwa na risasi tatu, ambayo inadaiwa kuporwa kwenye kampuni moja ya ulinzi ya ulinzi ya jijini Dar es Salaam.

Chanzo: ITV

Comments are closed.