POSHY AWAJIBU WANAOANDAMA SHEPU YAKE

Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’

BAADA ya madai kusambaa kuwa mrembo anayetingisha jiji kutokana na umbo lake namba nane, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ ametengeneza umbo nchini Afrika Kusini na kuwa na muonekano tofauti na alivyokuwa zamani, mwenyewe ametoboa kuwa ameamua kunyamaza kwa kuwa hakuna anayemlisha.

 

Akizungumza na Za Motomoto, Poshy alisema kuwa aliamua kunyamaza kwa sababu ameshangazwa sana na watu ambao wanavumisha hiyo skendo ya yeye kutengeneza shepu.

“Unajua nilinyamaza kwa sababu niliona wazi sina cha kuwaambia kabisa maana wao ndio wamekuwa wakinijua zaidi kuliko hata familia yangu. Kwanza picha wanazozisambaza ni za zamani wakati nikiwa mwembamba na si vinginevyo.

“Halafu kingine katika hilo kuna mambo mengi ya wivu na kutaka kuchafuana utaona hata ile picha wameitengeza nionekane sina kitu kabisa lakini mimi nimeachana nao kwa sababu hakuna mtu hata mmoja anayenilisha au kujua maisha yangu,” alisema Poshy.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment