The House of Favourite Newspapers

Prof. Joyce Ndalichako Akabidhi Mashamba na Vitendea kazi Kwa Vijana

0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) amekabidhi mashamba na vitendea kazi kwa vijana 268 waliopo kwenye programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) katika eneo la Chinangali- Dodoma, tarehe 22 Januari 2024.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo; Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Wakuu wa Taasisi za Wizara na Wadau utoke Benki za TADB na NMB.
“BBT ni kati ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia na niwahakikishie kama Waziri mwenye dhamana ya ajira na vijana, Serikali itaendelea kuwawezesha vijana katika programu hii endelevu.  Nyie kazi yenu kama vijana ni kushinda saiti na kuhakikisha mnazalisha kwa wingi,” amesema Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye  Ulemavu tarehe 22 Januari 2024 wakati wa hafla ya kukabidhi mashamba na vitendea kazi kwa vijana wa programu ya Build a Better Tomorrow- BBT.
Mhe. Prof. Ndalichako pia alishiriki katika zoezi la kupanda  miti.
Leave A Reply