The House of Favourite Newspapers

Prof. Tibaijuka Kurejesha Bilioni 1.6 za Escrow – Video

MBUNGE wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila (zilizoibua sakata la Escrow) ili aweze kutoka gerezani.

 

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha fedha hizo walizopokea ili kumsaidia mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

 

“Msamaha wa Rais unapotoka ni fursa adimu, sasa fursa ukiichezea utabaki kujuta mwenyewe,” amesema Profesa Anna Tibaijuka.

 

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa, Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

 

James Rugemarila, anatuhumiwa kwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Comments are closed.