The House of Favourite Newspapers

PSG na AS Roma Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Wijnaldum

0
Kiungo wa PSG Gini Wijnaldum

KLABU ya Paris Saint German ya nchini Ufaransa na AS Roma ya Italia imefikia makubaliano ya uhamisho wa kiungo raia wa Uholanzi Georginio Wijnaldum wa mkopo wa msimu mzima ambao una kipengele cha kumnunua kwa lazima kwa kiasi cha Euro milioni 10 mwishoni mwa mkopo wake.

 

AS Roma wanatarajia kukamilisha usajili wa kiungo huyo ikiwa ni baada ya kukamilisha dili la usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Argentina Paulo Dybala kama mchezaji huru.

Kabla ya kujiunga na PSG Wijnaldum alikuwa katika klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza

Wijnaldum alijiunga na PSG akitokea klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza na sasa ameamua kuondoka klabuni hapo kutokana nakushindwa kuendana na maisha ya soka katika klabu hiyo.

 

Aidha katika makubaliano baina ya vilabu hivyo ni kwamba PSG na AS Roma watashirikiana kulipa mshahara wa mchezaji huyo kwa pamoja kutokana na mchezaji huyo kuvuta mkwanja mrefu kwa mwaka.

 

 

 

Leave A Reply